BAREFOOT
Kituo cha wanawake cha kutengeneza umeme wa jua kimeazishwa Kibokwa- Kinyasini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutekeleza malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2020 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar.
SHUGHULI ZA KITUO
Kituo cha mafunzo ya utengenezaji wa vifaa vya umeme wa jua kwa wanawake kinajukumu la kutekeleza shughuli zifuatazo:-
- Kutoa mafunzo ya vitendo ya kutengeneza umeme wa jua kwa wanawake wa vijijini.
- Kuwahamasisha wanawake wa vijijini kujifunza na kuwafundisha wanawake wengine wa vijiji vya Zanzibar jinsi ya kuunganisha nishati ya umeme wa jua.
- Kuwahamasisha na Kuwawezesha wanawake wa vijijini juu ya kutafuta ajira na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kutumia nishati ya umeme wa jua.
- Kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kupata fursa za kuchangia ajenda mbali mbali za kitaifa juu ya kupunguza umasikini
- Kueneza umeme wa jua katika maeneo yote ambayo hayajafikiwa na huduma ya umeme unaotumia nguvu za maji ili kuimarisha hali na ustawi wa jamii katika maeneo hayo.
- Kuhamasisha na kukuza ushiriki wa wanawake katika fani za ufundi
- Kushawishi upatikanaji wa rasilimali watu na fedha za kutosha katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini juu ya kukiendeleza kituo.
Mbali na shughuli za msingi zilizotajwa hapo juu, Serikali imeona ipo haja ya kuongeza shughuli nyengine katika kituo hicho kama zifuatazo:-
- Kutoa ujuzi wa kushona nguo za aina mbali mbali kwa wanawake.
- Kutengeneza nguo za stara kwa ajili ya kuwasidia wanafunzi wakike kuendelea na masomo yao kwa vipindi vyote.
- Kuendeleza na kuboresha shughuli ya ufugaji nyuki.
Kwa maelezo zaidi, Tafadhali peruzi mtandao wetu wa barefoot Bonyeza hapa