KAMISHENI YA KAZI

Kamisheni ya Kazi itahusika na jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria za kazi na sera ya ajira ya Zanzibar.

Majukumu ya Kamisheni
  1. Kufanya ukaguzi kazi katika sehemu za kazi
  2. Kutatua migogoro ya kazi.
  3. Kukuza na Kuimarisha mahusiano mema kazini.
  4. Kupiga vita ajira za Watoto.
  5. Kuthibitisha Mikataba ya kazi.
  6. Kuwapatia Vibali vya Kazi vya wafanyakazi wa kigeni.
  7. Kuimarisha mahusiano na majadiliano ya Pamoja kazini.
  8. Kujenga uwelewa kwa jamii kuhusu sera, sheria za kazi na ajira Pamoja na mikataba ya kimataifa na kikanda inayohusiana na masuala ya kazi.
  9. Kusimamia utekelezaji wa Sheria za kazi nchini.
Kamisheni ya Kazi inavitengo vifuatavyo: -
  1. Kitengo cha Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro

    Kitengo hiki kinahusika na Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kazi.

    Majukumu ya Divisheni

    1. Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu masuala ya kazi na ajira
    2. Kupokea na kuratibu migogoro ya kazi (mashauri ya kazi) inayowasilishwa mbele ya Kitengo
    3. Kusuluhisha migogoro ya kazi (mashauri ya kazi);
    4. Kuamua migogoro ya kazi iliyoshindwa kusuluhishwa
    5. Kuratibu vikao vya Kamati ya Utatu (Tripartite Committee)
    6. Kuratibu na kuyapeleka mashauri yote yanayoitwa Mahakama Kuu (Industrial Court) kwa ajili ya kukaza hukumu (execution) na mapitio (review)
    7. Kutoa elimu kwa jamii na kufanya uchunguzi wa ufuatiliaji wa shughuli za Kitengo cha utatuzi wa migogoro ya kazi

  2. Kitengo cha Mahusiano ya Kazi na Viwango vya Kimataifa na Elimu Kazi

    Kitengo hiki kinasimamia utekelezaji wa Mikataba ya Shirika la kazi Duniani pamoja na kutoa elimu kuhusiana na mambo ya kazi.

    Majukumu ya Divisheni

    1. Kusimamia utekelezaji wa Mikataba ya Shirika la Kazi la Duniani kwa Taasisi za Serikali na Binafsi.
    2. Kuratibu na kuandaa ripoti ya utekelezaji wa Mikataba ya Shirika la Kazi kwa kushirikiana na Tanzania Bara katika kuiwakilisha nchini Geneva.
    3. Kuratibu na kuhakikisha ushiriki wa Tanzania Zanzibar katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa ya Shirika la Kazi Duniani na Mashirika yote yanayosimamia mambo ya Kazi.
    4. Kuaanda vipindi vya redio na televisheni kuhusiana na mambo ya kazi.
    5. Kutoa elimu juu ya Sheria za kazi katika Taasisi zote Zanzibar.
    6. Kuratibu mahusiano baina ya Kamisheni ya kazi Zanzibar na Wizara ya Kazi Tanzania bara katika mambo ya kazi.
    7. Kuratibu mawasiliano baina ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Wizara ya kazi katika mambo ya kazi.
    8. Kushughulikia ugeni wowote unaotoka mashirika ya ndani na nje katika mambo ya kazi kwa kamisheni ya kazi.

  3. Kitengo cha Kupambana na Ajira za Watoto.

    Kitengo hiki kinahusika na kuweka na kutekeleza mikakati ya kupinga Ajira za watoto Zanzibar.

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuratibu shughuli zote zinazohusiana na Ajira za watoto Zanzibar.
    2. Kuripoti mkataba No.138 unaohusu Umri wa Chini wa Kuajiriwa kwa Mtoto na mkataba No.182 unaohusu Ajira Mbaya kwa Watoto.
    3. Kutoa elimu juu ya athari za Ajira za Watoto Zanzibar.
    4. Kuwatoa watoto walio katika Ajira na walio katika hatari ya kuingia katika ajira hizo.
    5. Kuziwesha familia ambazo watoto wake wamo katika Ajira au wamo katika hatari ya kuingia katika Ajira hizo.

  4. Afisi ya Mrajis wa Vyama vya Wafanyakazi

    Afisi hii inasimamia Vyama vya Wafanyakazi na Jumuiya za Waajiri.

    Majukumu ya Afisi ya Mrajis

    1. Kusajili vyama vya Wafanyakazi na Waajiri kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
    2. Kutoa hati ya usajili kwa Chama au Jumuiya husika baada ya kujiridhisha na kuwa zimefuata utaratibu uliowekwa na Sheria ya Mahusiano Kazini No. ya mwaka 2005.
    3. Kufuta usajili wa chama kilichosajiliwa kwa maombi ya Chama au Jumuiya hiyo baada ya kuvunjwa kwake ikiwa Mrajis atathibitsha kwamba Jumuiya hiyo haifanyi kazi tena.
    4. Kusajili katiba au marekebisho ya katiba ya chama husika.
    5. Kupokea taarifa zilizokaguliwa kuhusiana na mapato na matumizi ya kila mwaka kutoka kwa kila Chama na Jumuiya.

  5. Afisi za Kazi Mikoa

    Afisi hizi zinasimamia utekelezwaji wa Sheria za Kazi nchini.

    Majukumu ya Afisi za Mikoa
    1. Kufanya ukaguzi kazi katika sehemu mbalimbali za kazi.
    2. Kuhakikisha raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini wa vibali vya kazi.
    3. Kufuatilia, kuchunguza na kuyapatia ufumbuzi malalamiko ya kazi kutoka kwa Waajiri na Waajiriwa.
    4. Kuthibitisha Mikataba ya Kazi.
    5. Kubainisha na kuwasilisha kwa Waziri mapungufu ya Sheria wakati wa usimamizi na utekelezaji wa Sheria za Kazi.