MAKABIDHIANO YA AFISI - ARKUU 11 March, 2024
Waziri wa Nchi - Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff amewataka watendaji wa Afisi hiyo kuwa tayari kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kuendana na kasi ya malengo ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya Afisi hiyo yaliyofanyika huko Afisini kwake Mwanakwerekewe Wilaya ya Magharibi B kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kumteuwa kuwa Waziri wa Afisi hiyo. Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya Afisi hiyo yaliyofanyika huko Afisini kwake Mwanakwerekewe Wilaya ya Magharibi B kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kumteuwa kuwa Waziri wa Afisi hiyo. Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya Afisi hiyo yaliyofanyika huko Afisini kwake Mwanakwerekewe Wilaya ya Magharibi B kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kumteuwa kuwa Waziri wa Afisi hiyo.
Makabidhiano hayo yamefanyika kati ya aliekuwa Waziri wa Afisi hiyo Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ambae kwa sasa ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Shariff Ali Shariff. Amesema matumizi ya teknolojia ni kitu muhimu kwa wakati tulio nao hivyo ni jambo muhimu kwa wafanyakazi kubadilika na kufanya kazi kwa kuzingatia haki na wajibu pamoja na kuzifuata Sheria za Utumishi kama zinavyoelekeza.
Aidha Mhe. Shariff ameahidi kuendelea kuwapa mashirikiano zaidi watendaji wa Afisi hiyo pamoja na kumshukuru Mhe. Rais kwa kumteuwa na kumuamini katika utendaji wake wa kazi Serikalini.
Nae, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhani Soraga amewataka watendaji kuwa watiifu kwa viongozi ili kumsaidia Mhe. Rais katika utendaji wake na kuendelea kumuamini kwa mabadiliko aliyoyafanya katika Afisi hiyo. Hatahivyo, amewasisitiza wafanyakazi kuwa makini katika kufanya kazi kwa ajili ya kufikia maendeleo katika nyanja zote ikiwemo kiuchumi na kijamii
Wakizungumza kwa niaba ya watendaji pamoja na wafanyakazi wa Afisi hiyo Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi na Uwezeshaji Bi Maryam Juma Abdulla na Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Uchumi na Uwekezaji Dkt. Habiba Hassan Omar wamesema wapo tayari kuendelea kumpa mashirikiano ya dhati Waziri huyo pamoja na kumshukuru Mhe. Soraga kwa wakati wote wa utendaji wake wa kazi kwani mafanikio yaliyopatikana ndani ya Afisi hiyo yanatokana na mipango na juhudi zake mbali mbali alizokuwa akizichukuwa wakati wa uongozi wake.
Imetolewa na;
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO.
AFISI YA RAIS, KAZI, UCHUMI NA UWEKEZAJI.