BODI ZA ARKUU

  1. Bodi ya Ushauri ya Mishahara

    Baadhi ya Kazi zake ni kama zifuatazo:

    1. Kutoa ushauri kwa Mheshimiwa Waziri wa masuala ya Kazi kuhusiana na malipo na punguzo la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya Utumishi wa Umma na wa Binafsi.
    2. Kumshauri Waziri wa mambo ya kazi juu ya kima cha chini cha mshahahara wa wafanyakazi na njia za kufikia kiwango hicho.
    3. Kutoa mapendekezo kwa Mheshimiwa Rais kuhusiana na viwango vya mishahara kwa makundi yote ya wafanyakazi wote wa Zanzibar.
  2. Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Kazi

    Baadhi ya Kazi zake ni kama zifuatazo:

    1. Kutoa ushauri kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu masuala ya Kazi kwa mujibu wa makubaliano ya Serikali ya Zanzibar na Shirika la Kazi Duniani ILO, ikiwemo kutoa maoni au dodoso na mapendekezo ya viwango vya kazi kimataifa, na uchukuaji wa hatua muhimu ili kwenda sambamba na masharti ya uanachama wa Shirika la Kazi Duniani, na mapendekezo ya malalamiko yoyote kuhusiana na mikataba iliyokwisha sainiwa (Ratified Conventions).
    2. Kushughulikia na kushauri kuhusu sheria yoyote iliyopendekezwa ambayo inaathiri kazi, uajiri, mahusiano kazini au mazingira ya Kazi.
    3. Kujadili masuala yoyote kuhusu kazi, uajiri, mahusiano Kazini na Mazingira ya kazi au sheria za kazi kwa mujibu watakavyoona inafaa, na kuripoti kwa maandishi kwa Mhe. Waziri kuhusu mjadala huo.
    4. Kumshauri Mhe. Waziri juu ya masuala yote kuhusiana na uajiri wa wafanyakazi, mahusiano ya kazi au umoja wa Waajiri au Waajiriwa kama itakavyo kama itakavyoelekezwa na Waziri.

    Kamisheni ya kazi inaongozwa na Kamishna wa kazi na imegawanyika katika vitengo vikuu saba (7).

    • Kitengo cha Utumishi, Mipango na Takwimu.
    • Kitengo cha Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro (DHU).
    • Ofisi ya mrajis wa vyama vya wafanyakazi na jumuiya za waajiri.
    • Kitengo cha kupambana na Ajira za Watoto.
    • Vitengo vya mikoa.
    • Kitengo cha Ukaguzi Elimu kazi.
    • Kitengo cha Mahusiano kazini na viwango vya kimataifa.
  3. Bodi ya Mamlaka ya Kukuza Uchumi Zanzibar (ZIPA)

    Ni chombo ambacho kinasimamia Uwekezaji Zanzibar.

    Majukumu ya Bodi ya ZIPA
    1. Kutoa maelekezo halali kwa Mkurugenzi Mtendaji katika utendaji, sera za utendaji na utekelezaji wa Mamlaka.
    2. Kuanzisha muundo wa taasisi na utaratibu wa kazi kama itakavyoona inafaa kwa utekelezaji wa kazi na majukumu ya Mamlaka.
    3. Kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma, kuainisha vigezo na masharti ya utumishi, mishahara na mafao kwa wafanyakazi wa Mamlaka.
    4. Kuweka mpango kazi, malengo na dhamira sahihi ya kazi kwa kila idara ya Mamlakana kusimamia hatua zilizofikiwa.
    5. Kuanisha mikakati au sera zinazoongoza utekelezaji Mamlaka.
    6. Kuteua kamati ambayo wajumbe wake watakuwa ni wale wale wajumbe wa Bodi au wajumbe wengine ambao imekasimu uwezo wake kadri itakavyoonekana inafaa.
    7. Kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma, kuanzisha kanuni za watumishi wa fedha.
    8. Kutoa miongozo ya ujumla katika sekta za kipaumbele za uwekezaji kwa kuzingatia maeneo yenye manufaa zaidi kwa Zanzibar.
    9. Kwa kuzingatia kanuni zitakazotungwa chini ya Sheria hii, kuidhinisha vigezo na viwango vya mtaji wa uwekezaji.
    10. Kufuatilia ipasavyo maendeleo ya Miradi iliyoidhinishwa.
    11. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 25(5) cha Sheria hii, kuthibitishwa ufutwaji wa Cheti cha Uwekezaji.
    12. Kuwa ni chombo cha mwanzo cha rufaa kwa Mwekezaji yeyote aliyeidhinishwa ambae hakuridhika na maamuzi.