IDARA YA UENDELEZAJI NA URATIBU WA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
Majukumu ya Idara
- Kutoa mafunzo ya uwezeshaji na ujasiriamali kwa wananchi ili elimu hiyo iweze kuingia katika mfumo rasmi wa elimu.
- Kueneza ujuzi na kutoa ushauri utakaosaidia wananchi kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato.
- Kufanya tafiti zenye lengo la kuandaa mipango itakayosaidia wajasiriamali kuingia na kuendeleza shughuli mbambali za kiuchumi ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
- Kutafuta rasilimali na Kukuza mifuko ya uwezeshaji, ili kusaidia wananchi kupata mitaji.
Idara hii ina Divisheni mbili (2) ambazo ni: -
-
Divisheni ya Mafunzo na Masoko
Divisheni hii itahusika na kutoa mafunzo na ukuzaji wa masoko kwa wajasiriamli itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Majukumu ya Divisheni
- Kutoa mafunzo ya uwezeshaji na ujasiriamali kwa wananchi
- Kuandaa mitaala na miongozo ya mafunzo ya kuwawezesha wananchi kiuchumi
- Kuwaunganisha wajasiriamali na masoko ya ndani na nje ya nchi
- Kuratibu maonesho mbali mbali ya wajasiriamamli
- Kuwaunganisha wajasiriamali na taasisi za viwango na ubora wa bidhaa
- Kufanya tafiti zenye lengo la kuandaa mipango
- Kuratibu na kuandaa tafiti za masoko
-
Divisheni ya Huduma za Uendelezaji wa Biashara na Ujasiriamali
Divisheni hii inahusika na uendelezaji wa biashara za wajasiriamali.
Majukumu ya Divisheni
- Kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya huduma na biashara
- Kusaidia ubunifu wa bidhaa na huduma mpya na kuongeza thamani
- Kuendeleza ubunifu wa technologia na vipaji vya wajasiriamali
- Uendelezaji na usimamizi wa vituo vya Uwezeshaji
DIRECTOR NAME
Director Title
Director Title