IDARA YA MAENDELEO YA VYAMA VYA USHIRIKA

Idara hii itahusika na majukumu ya usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar, Sheria ya Vyama vya Ushirika Zanzibar, na Kanuni zake ili kuviimarisha Vyama vya Ushirika na kuhakikisha kuwa vinaendeshwa kwa mujibu wa Sera, Sheria na Kanuni za Ushirika Ulimwenguni.

Idara hii itaundwa Divisheni tatu (3) ambazo ni: -
  1. Divisheni ya Maendeleo ya Ushirika

    Divisheni hii itahusika na majukumu ya usajili wa vyama vya ushirika, kutoa mafunzo na utatuzi wa migogoro ya vyama vya ushirika.

  2. Divisheni ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika

    Divisheni hii itahusika majukumu ya usimamizi wa vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi, kutoa miongozo na kusimamia ugavi na haki za wanachama.

  3. Divisheni ya Huduma za Fedha (SACCOS)

    Divisheni hii itahusika na usimamizi wa SACCOS ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria.