SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

AFISI YA RAIS KAZI UCHUMI NA UWEKEZAJI (ARKUU)

AFISI YA RAIS KAZI UCHUMI NA UWEKEZAJI (ARKUU)

DIRA

Kuwa na Jamii ya Wazanzibari inayojiweza, iliyoendelea na kuimarika kiuchumi.

DHAMIRA

Kuimarisha hali ya kijamii na kiuchumi ya wananchi wa Zanzibar kwa kutoa na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo na zitakazokuja, kushajihisha utamaduni na uwezo wa ujasiriamali, kukuza uwekezaji wa ndani na nje, upatikanaji wa kazi za staha na kuzingatia sheria na viwango vya kazi.

MALENGO

Afisi Ya Rais Kazi Uchumi Na Uwekezaji ilijiwekea malengo yafuatayo:-

  1. Kukuza na Kusimamia Uwekezaji kwa Maendeleo ya Nchi.
  2. Kubuni fursa za ajira nchini na kusimamia upatikanaji wa ajira za staha hasa katika Sekta Binafsi
  3. Kusimamia utekelezaji wa Mikataba ,Sharia na Kanuni za Kazi za kitaifa , Kikanda Na Kimataifa na kuimarisha mahusianio mazuri ya kazi miongoni mwa Serikali,Sekta Binafsi,Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi.
  4. Kuimarisha Usalama na Afya kazini.
  5. Kukuza na kusimamia Maendeleo ya Vyama vya Ushirika.
  6. Kukuza na kuimarisha mashirikiano baina ya Sekta Ya Umma Na Sekta binafsi.
  7. Kuratibu uandaaji na utekelezaji wa Sera ,Sharia ,Program Na Tafiti zinazohusiana na masuala ya Kazi ,Ajira ,Uwekezaji,Mashirikiano Baina Ya Sekta ya Umma Na Sekta Binafsi Na Uwezeshaji.
  8. Kuimarisha uratibu,mashirikiano,ufatiliaji na tathmini ya shughuliza Afisi pamoja na kuelimisha jamii juu ya shughuli za Afisi kupitia Mfumo wa TEHAMA.
  9. Kuimarisha ufanisi wa kiutendaji na maslahi ya Wafanyakazi wa Afisi

KANUNI ELEKEZI

  1. Mashirikiano katika kazi
  2. Uwajibikaji
  3. Uwazi
  4. Utaalamu katika utendaji kazi
  5. Uadilifu
  6. Ufanisi
  7. Uvumbuzi
  8. Usawa kwa wote
  9. Mjumuisho
Oganization Stucture