VITENGO VYA ARKUU
Muundo una vitengo sita (6) vilivyo chini ya Afisa Mdhamini vitengo hivyo ni kama vifuatavyo: -
- Kitengo cha Uhasibu
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya utayarishaji na ufanyaji malipo mbali mbali ndani ya Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji.
- Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya ushauri na udhibiti wa mali na fedha za Afisi, Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Afisi.
- Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma
Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ununuzi na na usimamizi wa uondoshaji wa mali za umma ndani ya Afisi.
- Kitengo cha Uhusiano
Kitengo hiki kitahusika na masuala ya mahusiano kati ya Afisi na taasisi nyengine, kuratibu malalamiko na kuzitangaza shughuli za Afisi.
- Kitengo cha Sheria
Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ushauri wa masuala ya kisheria katika Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji.
- Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano ndani Afisi ya Rais – Kazi Uchumi na Uwekezaji