IDARA YA MASHIRIKIANO BAINA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI

Idara hii itahusika na majukumu yafuatayo:

  1. Kupitia upembuzi yakinifu wa awali kwa miradi mikubwa na midogo.
  2. Kutoa ushauri na mapendekezo juu ya upembuzi yakinifu wa miradi iliyowasilishwa katika Idara ya PPP.
  3. Kupitia na kutoa mapendekezo ya maombi ya zabuni kwa miradi mikubwa.
  4. Kutoa elimu ya dhana na utekelezaji wa miradi ya PPP.
  5. Kupitia nyaraka za zabuni kwa miradi ya PPP
  6. Kufanya uchambuzi wa kifedha wa miradi na kupendekeza modeli bora ya mradi.
Idara inaundwa na Divisheni nne ambazo ni: -
  1. Divisheni ya Uchambuzi wa Kifedha kwa Miradi
    • Kutoa ushauri juu ya muundo mzuri wa kifedha wa miradi kwa kuzingatia taaluma ya thamani ya soko.
    • Kuchambua mifumo ya kifedha kwa kufanya uchambuzi yakinifu na dhana ya miradi inayowasilishwa ikiwa ni sehemu ya hatua za kiushindani na kuhakikisha miradi inatekelezeka na kuwa na thamani inayotarajiwa (value for money).
    • Kushauri Wizara/ Taasisi na mamlaka husika zinazotekeleza miradi ya PPP juu ya utafiti unaohitajika kuhakikisha miradi inatekelezeka.
    • Kuhakikisha kwamba Serikali inazingatia miradi kulingana na faida na gharama zake pamoja na mazingira hatarishi wakati wa upembuzi yakinifu na kufanya mawasiliano na wizara husika juu ya mambo hayo.
  2. Divisheni ya Sheria
    • Kufanya mapitio ya Sheria na kanuni wakati wa utayarishaji wa mradi.
    • Kutoa mapendekzo ya kisheria kwa miradi ya PPP
    • Kuandaa nyaraka za zabuni ya miradi.
    • Kufanya uchambuzi wa kisheria wa miradi.
    • Kupitia na kuandaa mikataba ya PPP.
    • Kutatua migogoro itakayojitokeza katika utekelezaji wa mashirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi.
  3. Divisheni ya Manunuzi
    • Kuandaa nyaraka za zabuni kwa kushirikiana na Divisheni ya Sheria na PMU ya Wizara.
    • Kupitia nyaraka za zabuni zinazoandaliwa na taasisi zenye miradi.
    • Kwa kushirikiana na taasisi zenye miradi, kuandaa mpango wa manunuzi wa miradi ya PPP.
    • Kushiriki katika kufanya tathmini ya zabuni kwa maombi ya miradi iliyowasilishwa kwa Taasisi zenye miradi.
    • Kuandaa mahitaji ya mradi na viashiria vyake.
  4. Divisheni ya Mapitio na Tathmini ya Miradi
    • Kutayarisha na kupitia nyaraka za kisheria kama vile taarifa za kisheria, makubaliano ya Sekta ya ubinafsishaji na nyenginezo kwa lengo la kuhakikisha maslahi ya Serikali yanalindwa.
    • Kushiriki kikamilifu katika hatua za zabuni na ufungaji wa mikataba wa miradi.
    • Kutoa elimu ya uhamasishaji juu ya mashirikiano baina ya Sekta Binasi na Sekta ya Umma.
    • Kuchambua aina zote za mazingira hatarishi kwa miradi na kuiweka katika mazingira yatakayopunguza risk.
    • Kuwashauri wadau wote wa PPP juu ya athari na aina za mazingira hatarishi ya miradi zinazoweza kutokea katika utekelezaji wa miradi hiyo.