IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

Idara hii inashughulikia na uandaaji wa mipango ya Afisi, bajeti, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi, kutayarisha na kuzifanyia mapitio Sera na kufanya tafiti za Afisi

Idara hii inaundwa na Divisheni Kuu nne (4) ambazo ni:
  1. Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini

    Divisheni hii itahusika na shughuli za ufatiliaji na ufanyaji wa tathimini wa mipango mbali mbali ya Afisi iliyopangwa kutekelezwa.

  2. Divisheni ya Maendeleo ya Sera

    Divisheni hii itahusika na shughuli za uandaaji na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoandaliwa na Afisi ili kuhakikisha zinakwenda sambamba na malengo yaliyokusudiwa.

  3. Divisheni ya Utafiti

    Divisheni hii itahusika na shughuli za ufanyaji wa tafiti mbali mbali na zinazohusu mipango, miradi na programu mbali mbali zinazoendeshwa na Afisi kuhusu sekta zinazosimamiwa.

  4. Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo

    Divisheni hii itahusika na shughuli za ukusanyaji wa taarifa na kutayarisha Mipango ya kisekta, kuandaa bajeti, kutayarisha taarifa ya utekelezaji.