KITUO CHA KULEA NA KUKUZA WAJASIRIAMALI ZANZIBAR

Utangulizi

Kituo cha ZTBI kinatoa huduma za ujasiriamali katika maeneo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Utalii (Tourism) na Usarifu wa Mazao (Agribusiness).

DIRA

Kuwa Kituo bora cha kuimarisha huduma za Tehama kwenye biashara na ujasiriamali Afrika Mashariki.

DHAMIRA

Kushajiisha uanzishaji wa Biashara Mpya na ukuaji wa Makampuni ya biashara ili yawe na Ukuaji Mafanikio Bora, yasimamiwe vyema na yawe na tija kwa faida ya Zanzibar.

MALENGO YA KITUO:

Kituo cha Kulea na Kukuza Wajasiriamali (Business Incubation Center) kina malengo mahsusi yafuatayo:-

  1. Kukuza na Kulea Wajasiriamali pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali vijana na wanawake ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
  2. Kuwapatia elimu juu ya upatikanaji wa masoko kwa bidhaa zao na kujenga mitandao.
  3. Kutoa Msaada wa kisheria wa kusajili biashara zao.
  4. Kupatiwa eneo la Ofisi ndani ya Kituo na fursa ya kutumia mashine kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa.
  5. Kufuatiliwa na kupewa miongozo ya kibiashara kuhusiana na masuala ya ujasiriamali na utengenezaji wa bidhaa.
  6. Kuwapatia mafunzo ya matumizi ya mashine na vifaa kwa ajili ya uzalishaji.
  7. Kuwaunganisha na huduma na fursa mbali mbali ikiwemo Mikopo (Revolving Fund)
  8. Kuwajengea uwezo vijana na wanawake ili waweze kupata fursa za kuchangia ajenda mbali mbali za kitaifa juu ya kupunguza umasikini.
  9. Kuhamasisha na kukuza ushiriki wa vijana katika fani za ufundi na ubunifu.
  10. Kushawishi upatikanaji wa rasilimali watu na fedha za kutosha katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini juu ya kukiendeleza kituo.

Kwa maelezo zaidi, Tafadhali peruzi mtandao wetu wa kituo cha kulea na kukuza wajasiriamali zanzibar Bonyeza hapa