IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI
Idara hii inahusika na utoaji wa huduma za uendeshaji na utumishi, kusimamia maslahi ya rasilimali watu, pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Afisi
Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:
- Divisheni ya Uendeshaji
Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Afisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
- Divisheni ya Utumishi
Divisheni hii itahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani Afisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi, upandishaji vyeo. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
- Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu
Divisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Afisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
MOHAMED JAFFAR JUMANNE
MKURUGENZI UENDESHAJI NA UTUMISHI
MKURUGENZI UENDESHAJI NA UTUMISHI