IDARA YA USALAMA NA AFYA KAZINI

Idara hii itahusika na majukumu ya usimamizi wa masuala ya afya na usalama katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi katika maeneo ya kazi, kuandaa kanuni na miongozo inayohusiana na afya na usalama katika sehemu za kazi.

Idara inaundwa na Divisheni tatu ambazo ni: -
  1. Divisheni ya Usalama Kazini

    Divisheni hii itahusika na masuala ya ukaguzi na uchunguzi wa mitambo, vifaa na zana za kunyanyulia vitu vizito.

  2. Divisheni ya Afya na Mazingira kazini

    Divisheni hii itahusika na masuala ya ukaguzi na uchunguzi mazingira ya Sehemu za kazi kwa jumla ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vyoo, maji safi na salama, hewa nzuri, mwangaza, mavumbi na kelele, afya za wafanyakazi na jamii inayozunguka sehemu za kazi, ajali na maradhi yatokanayo na kazi.

  3. Divisheni ya Usajili, Takwimu na Mafunzo

    Divisheni hii itahusika na kufanya usajili wa sehemu zote za kazi, utunzaji wa kumbukumbu zinazohusiana na sehemu za kazi kama vile ajali, kutoa takwimu na mafunzo yanayohusiana na afya na usalama kazini.