IDARA YA AJIRA

Idara hii itahusika na jukumu la usimamizi na utekelezaji wa sera ya ajira, mpango wa uzalishaji wa ajira na mpango wa utekelezaji wa ajira kwa vijana.

Idara inaundwa na Divisheni Kuu tatu (3) ambazo ni: -
  1. Divisheni ya Ukuzaji na Uundaji wa Ajira

    Divisheni hii itahusika na ukuzaji wa ujuzi kwa vijana (w’ke na w’me) ili waweze kukubalika katika Soko la Ajira, kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kujiajiri.

  2. Divisheni ya Takwimu za Ajira

    Divisheni hii itahusika na ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za ajira pamoja na kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana na ajira.

  3. Divisheni ya Huduma za Ajira

    Divisheni hii itahusika usimamizi wa taratibu za Soko la Ajira na kuhakikisha kwamba fursa za ajira zinapatikana kwa usawa na kwa wote pamoja na uratibu wa shughuli za uwakala wa ajira binafsi.