IDARA YA UENDELEZAJI NA URATIBU WA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

Majukumu ya Idara
  1. Kutoa mafunzo ya uwezeshaji na ujasiriamali kwa wananchi ili elimu hiyo iweze kuingia katika mfumo rasmi wa elimu.
  2. Kueneza ujuzi na kutoa ushauri utakaosaidia wananchi kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato.
  3. Kufanya tafiti zenye lengo la kuandaa mipango itakayosaidia wajasiriamali kuingia na kuendeleza shughuli mbambali za kiuchumi ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
  4. Kutafuta rasilimali na Kukuza mifuko ya uwezeshaji, ili kusaidia wananchi kupata mitaji.
Idara hii ina Divisheni mbili (2) ambazo ni: -
  1. Divisheni ya Mafunzo na Masoko

    Divisheni hii itahusika na kutoa mafunzo na ukuzaji wa masoko kwa wajasiriamli itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

    Majukumu ya Divisheni

    1. Kutoa mafunzo ya uwezeshaji na ujasiriamali kwa wananchi
    2. Kuandaa mitaala na miongozo ya mafunzo ya kuwawezesha wananchi kiuchumi
    3. Kuwaunganisha wajasiriamali na masoko ya ndani na nje ya nchi
    4. Kuratibu maonesho mbali mbali ya wajasiriamamli
    5. Kuwaunganisha wajasiriamali na taasisi za viwango na ubora wa bidhaa
    6. Kufanya tafiti zenye lengo la kuandaa mipango
    7. Kuratibu na kuandaa tafiti za masoko

  2. Divisheni ya Huduma za Uendelezaji wa Biashara na Ujasiriamali

    Divisheni hii inahusika na uendelezaji wa biashara za wajasiriamali.

    Majukumu ya Divisheni

    1. Kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya huduma na biashara
    2. Kusaidia ubunifu wa bidhaa na huduma mpya na kuongeza thamani
    3. Kuendeleza ubunifu wa technologia na vipaji vya wajasiriamali
    4. Uendelezaji na usimamizi wa vituo vya Uwezeshaji