WAKALA WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

DIRA

Kuwa kitovu chenye ufanisi cha kukuza/uwezeshaji wa biashara na uwekezaji kwa kutoa huduma bora kupitia kwa wataalamu waliohamasishwa wenye lengo la kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa Zanzibar na ustawi wa jamii.

DHAMIRA

Kuifanya Zanzibar kuwa kivutio cha kuvutia na chenye ushindani wa uwekezaji, kikanda na kimataifa

Majukumu ya ZEEF
  1. Kusimamia na kuendesha shughuli za Uwekezaji Zanzibar ikiwemo Maeneo Huru ya Uchumi kwa kuzingatia misingi ya uwazi na ushindani.
  2. Kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu yenye inayovutia kwa Uwekezaji, kituo cha biashara na eneo la usafirishaji.
  3. Kituo kikuu cha ushajihishaji, uwezeshaji, uwekezaji na biashara.
  4. Kutoa msaada wa kitaasisi kwa maendeleo ya kiuchumi na kuhakikisha uwekaji wa sera za kiuchumi na biashara.
  5. Kukuza, kuhamasisha na kuwezesha uwekezaji wa ndani au wa nje na kuhakikisha mazingira rafiki ya biashara.
  6. Kuwa ni taasisi kuu yenye kuhusika na kuitambulisha Zanzibar kiupekee katika kushajihisha uwekezaji.
  7. Kuwezesha uwekezaji wa ndani na wan je na kuhakikisha mazingira rafiki ya biashara.
  8. Kutoa msaada wa kitaasisi katika kuendeleza na kusimamia Maeneo Huru ya Uchumi.

Kwa maelezo zaidi, Tafadhali peruzi mtandao wetu wa Bonyeza hapa