Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff ameyasema hayo huko Ofisini kwake Mwanakwerekwe tarehe 11 Juni 2024 wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na siku ya kupambana na ajira za watoto, yanayofanyika kila mwaka ifikapo Juni 12.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa watoto wa kiume wanaathiriwa zaidi na masuala ya ajira za watoto hasa katika maeneo ya shamba.
Hivyo amesema Serikali inachukuwa hatua mbalimbali katika kushughulikia suala hilo ikiwemo kuanzisha Sheria ya Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011.
Aidha amesema, jumla ya watoto 53 wametolewa na kurejeshwa Skuli katika Shehia mbalimbali Kisiwani Pemba ikiwa ni pamoja na Shehia ya Mjini kiuyu, Maziwa ngombe, Wambaa, Mwambe na Kangagani.
Mbali na hayo ametoa wito kwa taasisi mbalimbali nchini, waajiri na wananchi wote kwa ujumla kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kukomesha ajira za watoto ili kuweza kuyafikia maendeleo endelevu ya Dunia “Suitanable Devolopment Goals {SDGs).
Jumla ya watoto 45,264 wameshiriki katika ajira za watoto ambapo asilimia 7.8 kati yao wana umri kati ya miaka 5 hadi 17.