Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff amefungua warsha ya siku tatu juu ya uandaaji wa Mfumo wa Soko la Ajira nchini (LMIS).
Warsha hiyo iliyofanyika leo tarehe 25 Juni 2024 huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip uliopo Uwanja wa Ndege Wilaya ya Magharib B iliyoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani kwa kushirikiana na Afisi yake ambayo imewashirikisha watendaji mbalimbali kutoka Taasisi za Umma na Binafsi.
Waziri Shariff amesema mfumo huo utasaidia kwa watunga sera na wafanya maamuzi katika kuweka mikakati ya kiuchumi kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.
Amesema katika kuusimamia na kuutekeleza mfumo huo kwa ufanisi Serikali kupitia Afisi yake inatarajia kuanzisha Sheria ya Ukuzaji wa Ajira (Employment Promotion Act) ambapo itaweka miongozo ya matumizi , uhifadhi na utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa maslahi ya umma.
Aidha, Mtaalamu wa Takwimu za Ajira kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO ) ndugu Maria Payet amesema mfumo huu utasaidia kupata taarifa mbalimbali kuhusu hali ya ajira kwa lengo la kuboresha hali za maisha nchini.
Nae Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Bi Maryam Juma Abdulla amewashukuru) kwa kushirikiana na Afisi yake katikamkuhakikisha uanzishwaji wa mfumo huo ambao utasaidia kuonesha fursa za ajira zilizopo nchini.
Zanzibar inatarajiwa kuwa nchi ya mwanzo kwa Afrika Mashariki kuwa na Mfumo wa Soko la Ajira (LMIS).